Mshambuliaji kutoka nchini Ubelgiji, Romelu Menama Lukaku, huenda akarejea Stamford Bridge baada ya kuwekwa kwenye orodha ya wachezaji watakaosajiliwa wakati wa majira ya kiangazi.

Lulaku ambaye kwa sasa anaitumikia klabu ya Everton, hakuwa na mustakabali mzuri ndani ya klabu ya Chelsea tangu kuwasili kwake huko magharibi mwa jijini London mwaka 2011 aikitokea nchini kwao Ubelgiji alipokua akiitumikia klabu ya Anderlecht, ameonekana kuwa kivutio tena, kutokana na juhudi na maarifa anayo yaonyeshwa kwa sasa.

Hata hivyo inadaiwa kwamba msikumo mkubwa wa Lukaku kupewa kipaumbele cha kurejea Chelsea, unatoka kwa mmiliki wa klabu hiyo Roman Arkadyevich Abramovich, anayedaiwa kuwa tayari kutoa mara mbili ya paund million 28, kama ada yake ya uhamisho.

Mkurugenzi wa ufundi wa Chelsea, Michael Emanalo amekua akifanya juhudi za kumrudisha Lukaku tena baada ya kuruhusu kuondoka jumla mwaka 2014.

Lukaku alitolewa kwa mkopo zaidi ya mara moja akiwa na klabu ya Chelsea ambapo kwa mara ya kwanza alipelekwa West Bromwich Albion katika msimu wa 2012–2013 na msimu uliofuata wa 2013–2014 alielekea Everton kabl ya kuondoka jumla mwishoni mwa msimu huo.

Chelsea wanajaribu kuongeza nguvu kwenye kikosi chao baada ya kuwa na msimu mbovu wa kutetea taji lao la ligi kuu ya soka nchini England (EPL).

Siku chache zijazo tunategemea kupata taarifa za klabu hiyo kuwa na meneja mpya kama mambo yatakwenda vyema.

Mabaliko haya ni ya lazima ikiwa Chelsea imetoka suluhu ya 1-1 dhidi ya Stoke City mwishoni mwa juma lililopita.

Hivi sasa The Blues wapo katika nafasi ya 10 katika msimamo wa ligi ya EPL wakiwa na points 40.

Azam FC Kuifuata Bidvest Sauzi J5
Utaupenda waraka huu kwa Rais Magufuli kuhusu Utumbuaji Majipu