Msanii Mkongwe wa Bongo Flava, Afande Sele ameeleza kuwa haoni sababu kwa wasanii wa Tanzania kwenda kufanya video zao Afrika Kusini wakati nchini kuna maeneo mengi. Amedai kufanya hivyo ni kuisaliti nchi.

Afande anaamini kuwa wanaoenda kufanya video zao nchini Afrika Kusini wanafanya ‘ulimbukeni’ na sio kwa sababu zenye mantiki ya kazi. “Kwenda kushuti video Afrika Kusini ni ulimbukeni,” Afande Sele aliiambia Bongo5.

Katika hatua nyingine, Afande amedai kuwa wanaoenda kufanya video zao Afrika Kusini wana biashara nyingine za siri zinazowasukuma kwenda nchini humo kwa mgongo wa kufanya kazi ya sanaa.

“Mimi hii naitafsiri ni usaliti wa nchi,  sisi tunakosa nini hapa nyumbani? Tuna milima, mbuga, maporomoko mazuri, yaani tuna kila kitu. Unajua wasanii wengi walikuwa wanatumia mwanya wa kwenda kushoot video nje ili kufanya biashara zao za siri. Wengi wameutumia sana huu mwanya, sasa Magufuli alivyoingia atawanyoosha tu,” Afande Sele amefunguka mtazamo wake.

50 Cent Amburuza Rick Ross Mahakamani
Jumamosi ya mwisho wa mwezi Yatangazwa kuwa Siku Maalum ya Usafi