Kiongozi wa kundi la G-Unit, 50 Cent ameripotiwa kumburuza mahakamani hasimu wake wa muda mrefu, Rick Ross akimtuhumu kutumia mdundo wa ngoma yake ya ‘In Da Club’ kuongeza umaarufu wa Mixtape yake ya hivi karibuni ya ‘Renzel Rimixes’.

Kwa mujibu wa TMZ, 50 Cent anataka Rick Ross amlipe fidia ya zaidi ya $ 2 million, kwa mujibu wa kesi aliyoifungua hivi karibuni dhidi ya rapa huyo.

Ingawa Rick Ross aliigawa bure mixtape yake hiyo, 50 Cent amedai kuwa mixtape hiyo ilitumiwa kama sehemu ya kuipigia debe au kuipa ‘kiki’ albam yake ya ‘Black Market’ iliyoachiwa wiki moja baada ya kutoka kwa mixtape hiyo.

50 Cent na Rick Ross wamekuwa na uhasimu wa muda mrefu ambao uliongezeka zaidi kwenye mitandao ya kijamii na kurushiana makombora kwenye mistari ya nyimbo zao. Bifu hiyo sasa inaonekana kuwafikisha rasmi kwenye vyombo vya dola.

Adai Kuzuiwa Kupanda Ndege Kwa Sababu Ni Muislam
Afande Sele: Kufanya Video Afrika Kusini ni Ulimbukeni