Kiungo wa klabu ya Arsenal Mohamed Elneny hatokua sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya Misri ambacho kitashuka dimbani kesho, kucheza mchezo wa nusu fainali ya michuano ya mataifa ya Afrika inayoendelea nchini Gabon.

Misri watapambana na Burkina Faso katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya michuano hiyo, ambao umepangwa kufanyika mjini Libreville.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24, bado anauguza majeraha ya kiazi cha mguu aliyoyapata wakati wa mchezo wa hatua ya robo fainali dhidi ya Morocco, ambao ulimalizika kwa Misri kuibuka na ushindi wa bao moja kwa sifuri.

“Elneny bado anasumbuliwa na maumivu ya kiazi chamguu. Na tunaendelea kusubiri taarifa ya daktari,” Alisema kocha Hector Cuper.

“Tunatarajia ataendelea kupata nafauu na ikiwezekana tumtumie katika mchezo wa hatua ya fainali, kama tutafanikiwa kupita kwa kuifunga Burkina Faso.”

Manolo Gabbiadini Kumalizana Na Southampton
CCM: Chadema wanasababisha migogoro ya ardhi