Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Monduli mkoani Arusha Loota Sanare, amesema halmashauri ya wilaya hiyo inayoongozwa na Chadema, inachochea migogoro ya ardhi na chama hakitakaa kimya kwa hilo.
Sanare ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara wa kijiji cha Lendikinya, uliohudhuriwa na vijana wa jamii ya Kimasai (morani) na wazee wa mila (Laigwanani) zaidi ya 300, kueleza ardhi ya kijiji hicho inayotaka kunyang’anywa na halmashauri hiyo.
Amesema kuwa vijana wa kimorani, Laigwanani na watu wengine akiwemo yeye mwenyewe Sanare, wanamiliki ardhi iliyopo katika kijiji hicho kwa kufuata michakato yote ya kisheria na hatimaye kupata hati ya kumiliki ardhi.
Aidha, amesema amesikitishwa sana na kauli ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, Isack Joseph kutangaza baadhi ya watu kuwa wanamiliki ardhi katika msitu huo kinyume cha sheria.
Hata hivyo,amesema kuwa si yeye tu anayemiliki ardhi katika kijiji hicho, kwani hata Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa (Waziri Mkuu mstaafu) ana ekari za kutosha katika eneo hilo pamoja na diwani wa Monduli Juu na wengine walioko ndani ya Chadema.
.

AFCON 2017: Mohamed Elneny Kuikosa Burkina Faso
Watford Wakataa Ombi La Odion Ighalo