Klabu ya Watford imekubali ofa ya Pauni milioni 20 iliyotumwa Vicarage Road kutoka mashariki na mbali (China) kwa ajili ya mshambuliaji Odion Ighalo.

Klabu ya Changchun Yatai inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini China, imetuma ofa hiyo ikiwa ni muendelezo wa dhamira iliyowekwa, ya kuwasajili wachezaji mashuhuri kutoka barani Ulaya na kwingineko.

Mshambuliaji huyo kutoka nchini Nigeria, aliwahi kuwaambia viongozi wa klabu ya Watford kuhusu uhamisho wake, ambapo aliwataka kumtoa kwa mkopo na si kumuuza moja kwa moja, lakini pendekezo lake halijasikilizwa.

Hata hivyo meneja wa Watford Walter Mazzarri anaamini kuondoka kwa Ighalo hakutomuharibia mipango yake, kutokana na kuwaamini M’Baye Niang na Mauro Zarate katika safu ya ushambuliaji.

Klabu ya West Brom ilikua imeonyesha nia ya kumsajili kwa mkopo mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27.

Ighalo anakabiliwa na changamoto ya kurejea katika kiwango chake kama ilivyokua msimu uliopita, kwani mpaka sasa ameshafunga bao moja katika michezo 18 ya ligi kuu ya soka nchini England aliyocheza.

CCM: Chadema wanasababisha migogoro ya ardhi
Video: Ugomvi wa DC, mbunge watua kwa Waziri Mkuu, Vijana wa CCM wamuonya Seif