Afisa wa Jeshi la maji la Uingereza ameripotiwa kuasi na kujiunga na kundi la Magaidi linalojiita Islamic States of Iraq and Syria (ISIS) nchini Syria.

Afisa huyo aliyetajwa kwa jina la Ali Alosaimi mwenye umri wa miaka 28, alichukua mafunzo ya jeshi la Maji katika moja ya vyuo mahili kwa mafunzo hayo nchini humo na anaelezwa kuwa na ujuzi wa hali ya juu katika operesheni za maji.

Wataalam wa jeshi la maji wameeleza kuwa hatua hiyo imeongeza hatari zaidi kwa Uingereza kushambuliwa kigaidi kwenye vyombo vya maji katika kipindi ambacho ISIS ilianza kulenga ndege za abiria na kutangaza mpango wa kuingiza wanajeshi wake wa maji kushambulia meli na feri za abiria.

Dailymail imeripoti kuwa taarifa za Alosaimi ambaye ni mzaliwa wa Kuwait zilipatikana katika nyaraka za kundi la IS zilizovuja kupitia barua pepe. Nyaraka hizi zilielezea wasifu wa Alosaimi kabla hajaondoka kuelekea nchini Syria kujiunga na kundi hilo.

Kwa mujibu wa taarifa za chuo alichochukulia mafunzo, Alosaimi alibobea katika masomo ya kuwa ‘deck officer’.

Deck Officers wana jukumu la kuangalia usalama wa meli, kupanga njia za meli, kupakia na kushusha mizigo pamoja na mawasiliano yote ndani ya meli,” kilieleza chanzo cha Dailymail.

Msichana wa miaka 9 aliyeokolewa mikononi mwa Boko Haram agoma kula, ataka arudishwe akaishi na ‘mumewe’
Mama Salma Kikwete amkingia kifua mumewe, ataka asilinganishwe