Mke wa Rais Mstaafu, Dk. Jakaya Kikwete, Mama Salma amewataka watanzania kuacha kufanya ulinganifu wa utendaji kazi wa Serikali iliyopita na Serikali iliyopo madarakani.

Akiongea katika Mkutano wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) hivi karibuni mjini Dodoma, Mama Salma alieleza kuwa yeye siku zote ataendelea kuisemea mambo mazuri serikali iliyopo madarakani.

Ingawa hakutaja majina, kauli yake inajieleza kutokana na kuwepo kwa wimbi la watu wanaousifia uongozi wa Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli na kuuponda uongozi uliopita.

“Kila mwaka naendelea kuisemea serikali iliyopo madarakani mambo mazuri, acheni hali ya kukaa na kuanza kusema kwamba serikali ile ilikuwa vile na serikali hii iko hivi. Wala msisema yule alikuwa vile na huyu yuko hivi, kwa kumalizia hayo napenda kusema mume wangu ambaye ni mwenyekiti wa CCM Taifa anawasalimia sana,” amesema Mama Salma.

Sio tu wananchi wa kawaida ambao wamekuwa wakilinganisha uongozi uliopita na uliopo, mwaka jana, Waziri wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano), January Makamba alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Nne ilijenga utamaduni wa kuleana na kuoneana haya. Kauli ambayo ilipingwa vikali na aliyekuwa Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Stephen Wasirra.

Katika hatua nyingine, Mama Salma alionesha kuunga mkono zoezi la utumbuaji majipu na kueleza kuwa Serikali ikimaliza kuyatumbua majipu katika ngazi za juu itahamia katika ngazi za chini. Aliwataka wote wanaojitambua kuwa ni majipu wajitumbue wenyewe mapema.

Afisa wa Jeshi la Uingereza ajiunga na magaidi wa ISIS, ana mafunzo ya hali ya juu
Machinga kutimulia kona zote Dar