Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, Ahmed Ally amewashukuru Mashabiki na Wanachama wa klabu hiyo kwa kumpokea vizuri.

Ahmed Ally alithibitishwa kuwa mkuu wa idara hiyo jana Jumatatu (Januari 03), kupitia kurasa za mitandao ya kijamii za klabu ya Simba SC.

Ametoa shukuruni hizo kwa Wanachama na Mashabiki wa Simba SC Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Kijamii wa Instagram ambapo ameandika: “Msemaji wa Mabingwa nimeamka salama Al hamdullillah.”

“Awali ya yote nisema asante Wana Simba kwa mapokezi makubwa niliyopata kutoka kwenu hii ni ishara kuwa mnanipenda, mnaniamini na mmenikubali nami niwahakikishie tuu sintawaangusha”

“Mapokezi yenu yamenipa nguvu, faraja na matumaini ya kuwa niko sehemu sahihi na sehemu salama, sehemu ya watu wenye upendo wa hali ya juu hakika hii sio timu hii ni Familia,” Ofisa Habari wa Simba SC.

Young Africans yaelekea Zanzibar
Mkwasa arudi Ruvu Shooting