Meneja wa Habari na Mawasilino Simba SC Ahmed Ally ametangaza rasmi kuzifunga sherehe za ushindi wa mchezo wa Mzunguuko wanne wa Kundi C, Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Vipers SC.

Simba SC ilichomoza na ushindi wa 1-0 dhidi ya Mabingwa hao wa Uganda juzi Jumanne (Machi 07), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, bao likifungwa na kiungo kutoka nchini Zambia Clatous Chotta Chama.

Ahmed ametumia kurasa zake za Mitandao ya Kijamii kutoa taarifa za kufungwa kwa sherehe za ushindi huo, huku akithibitisha kufunguliwa kwa mlango wa hamasa ya mchezo wa Mzunguuko watano dhidi ya Horoya AC ya Guinea, utakaopigwa Jumamosi (Machi 18), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Ahmed Ally ameandika: Rasmi tumemaliza sherehe za kumfunga Vipers, leo tunaanza mipango ya kumfunga Horoya

Mechi yetu na Horoya ni Jumamosi March 18 saa 1:00 Usiku tukishinda mchezo huo moja kwa moja tunatinga Robo Fainali

Maandalizi ya kiufundi tuwaachie wataalamu, Sisi mashabiki tuanze maandalizi yetu ya kuujaza Benjamini Mkapa

Kila mwana Simba ana wajibu wa kuisaidia Simba kutinga Robo Fainali msimu huu

Hamasa zianze sasa kwenye Matawi, Mitaaa, Masoko pamoja na Makundi yetu ya wastup kuhakikisha kwamba hakuna Mwana Simba anabaki nyumbani siku iyo

Mpango wa hamasa kitaifa tutautangaza punde tuu baada ya mechi ya Mtibwa Sugar

Tuungane pamoja kuipeleka Simba Robo Fainali

GGML Ladies watoa vifaa tiba kwa akina mama Wajawazito
Mkutano LDC5 waangazia mchango wa wanawake Kiteknolojia