Jamii imeshauliwa kutafuta fursa za kiuchumi kupitia mitandao ya simu za mikononi ikiwa ni pamoja na kurahisisha shughuli zao za kiuchumi kwa kutafuta masoko ya bidhaa mbalimbali badala ya kutumia mitandao hiyo kwa ajili ya mawasiliano yasiyo na tija.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa huduma za jamii jijini Arusha, Isaya Doita mara baada ya kuzindua duka la huduma za mkononi kutoka kampuni ya Airtel lililopo Ngarenaro.
Amesema kuwa pamoja na nchi kupiga hatua katika teknolojia ya mawasiliano lakini bado wananchi hawajaweza kutumia vizuri mitandao hiyo kukuza uchumi wao.
Hata hivyo, kwa upande wake Meneja wa Airtel Kanda ya Kaskazini, Benson Bwanga amesema kuwa wameona umuhimu wa kuisaidia jamii kurahisha shughuli zao hasa katika suala la usalama uhamishaji fedha.