Abiria wanne, waliokuwa wakisafiri na basi la Kampuni ya Happy Nation, wamejeruhiwa katika ajali, huku wengine 37 wakinusurika kifo baada ya basi walilokuwa wakisafiria kugongana na lori aina Lori eneo la Mkambarani Mkoani Morogoro.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Morogoro, ACP Ralph Meela amesema chanzo cha ajali hiyo iliyotokea hii leo Julai 20, 2022 majira ya saa 3:00 asuhubi ni uzembe wa dereva wa basi aliyekiuka sheria za usalama barabarani kwa kujaribu kuyapita magari mengine bila tahadhari.

Basi la Kampuni ya Happy Nation, lililopata ajali kwa kugongana na lori aina Lori eneo la Mkambarani Mkoani Morogoro hii leo Julai 20, 2022.

Ajali hiyo, imehusisha basi la Happy Nation lenye namba za usajili T 702 DGF likilokuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Bukoba na lori la mizigo lenye namba za usajili T179 DCR aina ya Scania lililokuwa likitokea Zambia kuelekea Mkoani Dar es Salaam.

Baadhi ya abiria waliokuwa kwenye basi hilo, wamesema wameliomba jeshi la Polisi kitengo cha Usalama Barabarani kuongeza umakini katika utendaji wao kwa kuwachukulia hatua madereva wazembe ili kupunguza ajali zisizo za lazima.

Basi la Happy Nation lililopata ajali ya kugongana na Lori na kusababisha majeruhi wanne.

Simon Msuva: Ninawashukuru sana watanzania wenzangu
Waliochaguliwa kidato cha kwanza washindwa kuripoti shule