Jumla ya Wanafunzi 76, waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2022 katika Shule tatu za Sekondari zilizopo Wilayani Urambo Mkoani Tabora, hawajaripoti kuanza masomo.

Ofisa Elimu Sekondari Wilaya ya Urambo, Philipo Balugahale ameyasema hayo mbele ya Mbunge Urambo Margaret Sitta, katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata tatu za mji mdogo wa Urambo Mchikichini, Kiyungi na Urambo.

Wanafunzi wakitoka Shuleni.

Amesema, Idara ya Elimu ilifanya jitihada za kuitisha mikutano mbalimbali ya Wazazi kuwataka wawapeleke watoto wao shule bila mafanikio.

Shule ambazo mpaka sasa Wanafunzi wake hawajaripoti ni Chetu Wanafunzi 19, Ukombozi Wanafunzi 45, na Shule ya Sekondari Urambo Day wanafunzi 12.

Ajali ya basi na Lori, 41 wanusurika kifo
Kamati kufuatilia utendaji wa majeshi kuundwa