Hali ya taharuki imezuka katika mtaa wa Fungafunga kata ya Kichangani Manispaa ya Morogoro, baada ya Mtu mmoja mwanaume ambaye jina lake halikufahamika mara moja amekutwa mefariki huku mwili wake ukielea kwenye dimbwi la maji.

Wananchi katika eneo hilo waliofika kushuhudia tukio.

Mwenyekiti wa mtaa wa Fungafunga, Thabiyi Mgalula amesema alipokea taarifa kutoka Kwa wananchi kua kuna mwili wa mtu ukielea kwenye dimbwi la maji ambalo limetokana na ufyatuaji matofali ndipo akatoa taarifa Jeshi la Polisi.

Dimbwi la maji alipoktwa mtu huyo akiwa amefariki.

Kaimu kamanda wa jeshi la zimamoto na uokoaji, Emanuel Ochieng amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kwa sasa mwili huo utapeleka hospitli ya Rufaa Mkoa Morogoro Kwa ajili ya uchunguzi wa chanzo cha kifo pamoja na utambuzi.

Mhadhiri ataka ushirikishwaji wa jamii matukio ya uhalifu
Wataalamu kuibua ajenda miradi ya mazingira