Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Elija Kondi amesema ujenzi wa uelewa wa pamoja baina ya Jeshi la Polisi na Serikali za mitaa utasaidia kufanikisha suala la ushirikishwaji wa jamii katika kufichua vitendo vya kihalifu.

Kondi ameyasema hayo wakati akiongea na Watendaji wa Kata pamoja na Wakaguzi wa Kata za Jiji la Arusha, tukio lililofanyika katika ukumbi wa mikutano ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji na kuongeza kuwa watendaji hao wanatakiwa kukemea vitendo vya kihalifu, hasa vile vya ukatili wa Kijinsia.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Hargeney Chitukuro amesema uongozi wa Jiji hilo utahakikisha unaboresha mazingira ya kiutendaji baina ya Polisi kata na Watendaji wa kata ili dhana nzima ya Polisi jamii ilete matokeo chanya katika kata zote za jiji la Arusha.

Jeshi la Polisi Nchini, kupitia Kamisheni ya Polisi jamii lipo katika ziara ya kuzunguka Nchi nzima kujenga uelewa wa pamoja baina yake na Kamati za ulinzi na usalama Mikoa na Wilaya zote pamoja serikali za mitaa, kuhusu suala zima umuhimu wa kushirikisha jamii kufichua matukio ya uhalifu.

Serikali yasisitiza ukaguzi utekelezaji miradi ya maendeleo
Akutwa amefariki katika dimbwi la maji