Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Dkt. Ibenzi Ernest ameelezea mafanikio yaliyopatikana kwenye Hospitali hiyo katika kipindi cha miaka miwili, baada ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, kuandaa programu maalumu ya kutangaza mafanikio ya Serikali kwa Taasisi zilizopo Mkoani humo.

Akiongelea mafanikio hayo, Dkt. Ibenzi amesema Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma inajivunia kuwa miongoni mwa Hospitali za Rufaa za Mikoa nchini zenye utoaji wa huduma bora za mifupa na uboreshaji wa misingi ya kutoa huduma kwa wagonjwa.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Ibenzi Ernest akielezea mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kipindi cha miaka miwili madarakani katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa jengo la Mkapa.

“Tumeboresha misingi ya kutoa huduma kwa wagonjwa wetu na tuna mpango wa kufanya huduma za afya ziwe za kitalii zaidi kwani tunataka mikoa mingine iweze kutoa huduma kama zetu. Tunalenga kwenye utoaji wa huduma bora,” amesema Dkt. Ibenzi

Kuhusu vipimo vya mionzi, Dkt. Ibenzi amesema Hospitali imeongeza vipimo vya mionzi kutoka viwili hadi kufikia 7, vipimo vya Ex-Ray vitatu kutoka kimoja cha awali pamoja na kipimo cha CT-SCAN kwa sasa kinapatikana hospitalini hapo.

Wataalamu kuibua ajenda miradi ya mazingira
Uhalifu: Kamishna awakutanisha Watendaji, Polisi Kata