Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali imefanya kazi kubwa ya kuhakikisha inatekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi, hivyo ni jukumu la viongozi kuikagua na kujiridhisha kama utekelezaji wake unafanyika kwa viwango vilivyokusudiwa na unalingana na thamani halisi ya fedha iliyotolewa.

Majaliwa, ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi katika eneo la Kakozi wilayani Momba akiwa kwenye ziara ya kikazi mkoani Songwe ya kukagua miradi ya maendeleo na mafanikio ambayo Serikali ambayo imeyapata katika kipindi cha miaka miwili.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea maelekezo ya mradi wa kimkakati.

Kabla ya kuzungumza na wananchi, Waziri Mkuu alikagua ujenzi wa mradi wa kimkakati wa soko la Kimataifa la mazao ya kilimo na mifugo pamoja na maghala sita ambapo alisema ameridhishwa na hatua iliyofikia na kuupongeza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba kwa utekelezaji wa miradi hiyo.

Mradi huo wenye thamani ya shilingi bilioni 8.6, unatekelezwa kwa fedha kutoka Serikali Kuu, pia unahusisha ujenzi wa mnada wa kuuzia mifugo, josho, kukamilika kwa mradi huo kutaongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani ya halmashauri hiyo na hivyo kuwezesha ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya kutolea huduma za jamii.

NEEC yatoa mikopo ya Trilioni 5.6 kwa Wananchi
Mhadhiri ataka ushirikishwaji wa jamii matukio ya uhalifu