Magwiji wa soka nchini Misri, klabu ya Zamalek ipo katika mchakato wa kumsaka mkuu wa benchi la ufundi, baada ya aliyekua akishika nafasi hiyo Moamen Soliman kufanya maamuzi ya kujiuzulu mwishoni mwa juma lililopita.

Klabu ya Zamalek ambayo ilimaliza michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika kama mshindi wa pili baada ya kufungwa na Mamelodi Sundowns majuma mawili yaliyopita, ilipoteza mchezo wa ligi siku ya ijumaa kwa kufungwa bao moja kwa sifuri dhidi ya Al Masry.

Kitendo cha kufungwa katika mchezo huo, kilikua chanzo kwa Soliman kuondoka klabuni hapo, baada ya kufanya kikao na mwenyekiti  Mortada Mansour ambaye alivieleza vyombo vya habari kusikitishwa na hatua ya kuzikosa point tatu muhimu dhidi ya Al Masry.

Image result for Moamen Soliman on sky sportsMoamen Soliman

Mpaka sasa haifahamiki katika kikao cha wawili hao jambo gani lilizungumzwa hadi kufikia Soliman kutangaza kujiuzulu nafasi yake ya ukocha mkuu.

Soliman, alikabidhiwa jukumu la kuwa kocha mkuu wa Zamalek mwezi Agosti mwaka huu, na alikiongoza kikosi cha The White Knight hadi kutwaa ubingwa wa kombe la Misri na kisha aliwapeleka katika hatua ya fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika kabla ya kufungwa na Mamelodi Sundowns.

Msimamo wa Rais Magufuli wamchanganya Lissu
Magufuli atuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Spika Mstaafu, Samweli Sitta