Rais wa klabu ya Corinthians ya nchini Brazil, Robero de Andrade ameshindwa kujizuia na kujikuta akitoa siri nzito iliyokua imejificha dhidi mshmabuliaji Alexandre Pato.

Andrade, amesema uongozi wa klabu ya Liverpool unakaribia kumsajili Pato, baada ya mazungumzo kwenda vizuri na kilichosalia ni hatua chache ambazo zitamuwezesha mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26, kuelekea nchini England mwezi januari mwaka 2016.

Amesema jambo kubwa lililokua likiendelea kati ya viongozi wa pande hizo mbili ni kufikiwa kwa makubaliano ya usajili wa mshambuliaji huyo ambaye aliwahi kuitumikia klabu ya AC Milan ya nchini Italia, na sasa wamempa ruhusa Pato kukamilisha makubalino binafsi ya kimaslahi na viongozi wa klabu ya Liverpool.

Hata hivyo Andrade, amekiri wazi kwamba Pato alikua anawindwa na klabu za Tottenham pamoja na West Ham Utd zote za nchini England, lakini Liverpool wameonyesha kuwa tayari kukamilisha dili kwa ada kubwa ya usajili.

Kama itakumbukwa vyema miezi miwiwli iliyopita Pato, alifichua siri ya kutaka kusajiliwa na Man Utd katika siku ya mwisho ya usajili wa majira ya kiangazi lakini alikataa, hivyo taarifa za kuwa mbioni kujiunga na Liverpool mwezi januari huenda zikadhihirisha rasmi alikua hapendezwi na wito wa mashetani wekundu.

Hatma ya Babu Seya na Mwanae Kuamriwa Mahakama ya Afrika
Q Chief Atangaza Ndoa