Q-Chief amepanga kufunga pingu za maisha na mrembo wake aliyedumu naye kwa muda mrefu baada ya kuona kuwa anafaa kuwa mkewe wa maisha.

Mwimbaji huyo ameiambia EATV kuwa anaendelea na maandalizi ya harusi yake hiyo itakayofanyika Januari 2016.

Mwimbaji huyo alisema kuwa amemuandalia mkewe mtarajiwa zawadi nzuri ya wimbo maalum kwa ajili yake.

“Ni mwanamke msitahimilivu ambaye amenipa moyo katika kipindi kigumu kwahiyo nikasema hapana ngoja nifanye kitu kwa niaba yake kwahiyo hii ni zawadi yake,” alisema Q-Chillah.

Alexandre Pato Kucheza Soka England
Malinzi Atoa Pongezi Kwa Samatta Na Ulimwengu