Mgombea ubunge wa jimbo la Mtama, Nape Nnauye ambaye pia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM amezungumzia ajali mbaya ya gari aliyoipata jana usiku alipokuwa njiani akitokea Dar es Salaam kuelekea Lindi.

Nape ameeleza kuwa yuko salama na alipata majeraha madogo ingawa ajali hiyo ilikuwa mbaya kwa kuwa gari lake lilipinduka na kueuka mara kadhaa baada ya tairi ya mbele ya gari lake aina ya Land Cruiser alilokuwa anaendesha kupasuka.

Gari alilopata nalo ajali, Nape Nnauye

Gari alilopata nalo ajali, Nape Nnauye

“Namshukuru Mungu nimetoka salama na nawaomba wananchi wasiwe na hofu japo ajali ilikuwa mbaya maana gari lilipinduka mara kadhaa, nimepata majeraha madogomadogo na michubuko ila ni mzima,” alisema Nape.

Mgombea huyo wa ubunge alikuwa peke yake kwenye gari hilo na ameeleza kuwa mkanda na ‘air bag’ zilimsaidia kupunguza makali ya ajali hiyo.

“Gari limeharibika vibaya ila ninachoshukuru nilikuwa nimefunga mkanda na ‘air bag’ nazo zimenisaidia,” alisema.

Dar24 inampa pole kwa ajali iliyompata, apone haraka majeraha madogo aliyonayo.

Louis van Gaal: Anthony Martial Ni Mpumbavu
Mchezaji Wa Simba Akutwa Na Begi Uwanjani