Mshambuliaji wa Simba, Pape N’daw raia wa Senegal ametoa kali ya mwaka baada ya kugundulika ana bonge la hirizi katikati ya mechi.

N’daw raia wa amekutwa akiwa na hirizi kubwa iliyowashitua wachezaji wa Prisons wakati mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, leo.

Wakati mechi inaendelea, mabeki wa Prisons walianzisha tafrani kubwa wakidai N’daw ana hirizi tena ni kubwa kuzidi hata ngumi yake.

Hali hiyo ilizua mzozo mkubwa uwanjani hapo, baadaye wachezaji hao walivuta jezi yake na kugundua kweli alikuwa na hirizi.

Baada ya wachezaji wa Simba kuona kweli N’daw alikuwa na hirizi, walishindwa hata kumtetea na kumuacha mwamuzi achukue uamuzi.

Mwamuzi wa mchezo huo aliamua kumtoa nje N’daw ili akashushe ‘mzigo’ wake huo na baadaye kurudi uwanjani.

Mechi hiyo ilikuwa ni ya kwanza kwa N’daw kuanza katika 11 bora. Lakini ameshindwa kuonyesha uwezo kisoka.

Alichokisema Nape Baada Ya Kupata Ajali Mbaya Ya Gari
Waweka Magari na Nyumba Rehani Kutabiri Rais Ajaye , Ni Rukhsa Kushiriki