Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhajj Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewahimiza Waumini wa Dini ya Kiislamu kuendelea kuitunza amani na kudumisha umoja pamoja na mshikamano wa watu nchini.
Rais Dkt. Mwinyi amesema hayo alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika Msikiti wa Masjid Kheir Batini Nyamanzi, Wilaya ya Magharibi B Mkoa wa Mjini Magharibi hii leo Novemba 10, 2023.
Aidha Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa amani ya nchi ni jambo la msingi la kwanza huku akitoa pole kwa wananchi waliopata maafa kwa mvua zilizonyesha hivi karibuni, na kuwakumbusha kwamba ni wajibu kumuomba Mwenyezi Mungu kwa mvua zenye neema.