Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Italia, Antonio Conte, amesisitiza kutumia mfumo wa 4-4-2, katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Ublegiji ambao umepangwa kuchezwa hapo kesho.

Conte amesisitiza kutumia mfumo huo, ikiwa ni sehemu ya mipango yake tangu alipokubali kukifundisha kikosi cha The Azzurri, August 14 mwaka 2014.

Mfumo huo umekua ukimsaidia conte kutengeneza ukuta mgumu katika safu ya ulinzi kwa kuwategemea mabeki wanne na viungo wanne huku washambuliaji wawili wakipambana kusaka ushindi.

Hata hivyo msisitizo wa Conte, umetolewa ufafanuzi na baadhi ya vyombo vya habari nchini Italia, ambapo imeaminika kwamba pamoja na kutarajia kuwatumia washambuliaji wawili ambao ni Eder na Graziano Pellè, pia atawatumia viungo Antonio Candreva na Alessandro Florenzi kucheza pembeni.

Katika mchezo huo wa kesho, Conte anatarajia kumchezesha kiungo Claudio Marchisio WA Juventus, ambaye alikua majeruhi sambamba na Marco Parolo wa klabu ya Lazio.

Mapacha wa Juventus Giorgio Chiellini na Leonardo Bonucci wanatarajiwa kuwa katika safu ya ulinzi kwa usaidizi wa Matteo Darmian wa Man Utd pamoja na Mattia De Sciglio wa AC Milan.

Kikosi ambacho kinatarajiwa kuanza dhidi ya Ublegiji hapo kesho kwa mfumo wa 4-4-2 ni Buffon; Darmian, Bonucci, Chiellini, De Sciglio; Candreva, Parolo, Marchisio, Florenzi; Eder, Pellè.

Mfumo wa 4-4-2, umeonyesha mafanikio makubwa kwa kocha huyo ambaye aliweka heshima kwenye klabu ya Juventus kwa kutwaa ubingwa wa Italia mara mbili mfululizo, kwenye michezo ya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya barani Ulaya za mwaka 2016.

Cesc Fabregas Ajitahidi Kusafisha Hali ya Hewa
Video: Mrembo atembea ‘Mtupu’ Katikati ya Jiji Bila Kushtukiwa