Kiungo kutoka nchini Hispania, Francis Cesc Fabregas ameshangazwa na madai yanayotolewa na wadau wa soka duniani, kuhusu ushirikiano uliopo kati ya wachezaji wa klabu ya Chelsea dhidi ya meneja wao Jose Mourinho.

Fabregas, ambaye alisajiliwa na Chelsea msimu uliopita akitokea FC Barcelona kwa ada ya uhamisho wa Euro million 33, amesema madai yanayotolewa ya kuwepo kwa ushirikiano hafifu baina ya pande hizo mbili sio ya kweli na yana lengo ya kuupotosha umma wa mashabiki wa The Blues.

Fabregas, amesema pamoja na hali kutokua nzuri kwenye kikosi chao kufuatia matokeo mabaya waliyoyachuma mpaka sasa, bado kuna ushirikiano mzuri baina ya wachezaji dhidi ya meneja Mourinho.

Amesema kuna hali ya kuaminiana kwa kila mmoja tangu wanapokua mazoezini hadi wanapofika kwenye michezo ya kimashindano, na amesisitiza kinachotokea uwanjani ni matokeo ya soka ambayo huweza kuipata timu yoyote duniani.

Hata hivyo kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28, ameonyesha kuwa na matumaini makubwa ya kuendelea kumuona Mourinho akifanya kazi zake kwa ustadi mkubwa huko Stamford Bridge, licha ya kuwepo kwa tetesi za kuwa hatarini kutimuliwa.

Fabregas amekua mmoja wa wahezaji wanaotupiwa lawama na baadhi ya mashabiki, kwa madai ya kushindwa kufanya wajibu wake anapokua uwanjani, kama alivyozoeleka akiwa Arsenal pamoja na FC Barcelona na wakati mwingine anatajwa kufanya mambo hayo kwa makusudi.

Chelsea tayari wameshapoteza michezo saba katika mwenendo wa ligi ya nchini England msimu huu, wameshinda mara tatu na wametoka sare mara mbili, hali ambayo inawaweka kwenye nafasi ya 16, katika msimamo.

Raheem Sterling: Sijutii Kuondoka Liverpool
Antonio Conte Kuendelea Kuutumia Mfumo Wa 4-4-2