Mwanamitindo mmoja mrembo ametembea akiwa mtupu katikati ya jiji la Hong Kong, China bila kushtukiwa na watu waliokuwa wakimuona.

Mrembo huyo alikuwa amevaa fulana fupi pekee mwili mwake huku akiwa amechorwa mfano wa ‘jeans’ kuanzia kiunoni hadi miguuni, hali iliyowafanya wapita njia wengi kudhani amevaa ‘jeans’.

Model

Msichana huyo alichorwa kwa ustadi na msanii maarufu wa michoro aitwaye Sandra Bakker.

Video iliyosambazwa mitaani ilimuonesha msichana huyo akipita katika mitaa yenye msongamano wa watu na maduka makubwa ya manunuzi.

Treni

Hata hivyo, aliwashtua wengi baada ya kubainisha alichovaa mwilini kwa kuonesha maandishi kwenye fulana yake iliyosomeka, “No pants are the best pants’.

Antonio Conte Kuendelea Kuutumia Mfumo Wa 4-4-2
Matunda ya Ziara za Kushtukiza za Rais Magufuli Haya Hapa