Ziara za kushtukiza za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli zimezaa matunda katika hospitali ya Muhimbili na Ofisi nyingine za Serikali.

Baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kukuta mashine za MRI na CT – Scan hazifanyi kazi, uongozi wa hospitali hiyo umetangaza jana kuwa mashine ya MRI imetengenezwa tayari na imeanza kazi.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha hospitali hiyo, Aminiel Aligaesha, mashine hiyo imeanza kufanya kazi jana majira ya saa tisa alasiri.

“Menejimenti inapenda kuutangazia umma kwamba mashine aina ya Magnetic Resonance Imagine (MRI) imeanza kufanya kazi majira ya saa tisa alasiri November 11, 2015 mara baada ya mafundi wa Phillips kuifanyia matengenezo kuanzia mchana wa leo (jana).”

CT SCAN

Aliongeza kuwa juhudi zaidi zinaendelea kuhakikisha wanakamilisha utengenezaji wa mashine ya CT-Scan kama ilivyoelekezwa na Rais.

Katika hatua nyingine, ziara ya Rais katika wizara ya fedha imezaa matunda sio tu kwenye ofisi za wizara hiyo bali katika ofisi zote za serikali ambapo taarifa zinaeleza kuwa mahudhurio na utaratibu wa kufuata ratiba ya kuwahi kazini na kufanya kazi unafuatwa kwa kiwango kinachoridhisha.

 

 

Video: Mrembo atembea ‘Mtupu’ Katikati ya Jiji Bila Kushtukiwa
Ancelotti: Nipo Tayari Kumpokea Mzigo Jose Mourinho