Msafara wa watu 33 ikiwa ni wachezaji 24 na viongozi 9 wa klabu ya As Vita Club umeanza Safari ya kuelekea jijini Dar es salaam na wanatarajia kufika nchini Tanzania Usiku wa Saa 1:00.

AS Vita wanakuja kucheza mchezo watano wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika hatau yaMakundi dhidi ya wenyeji wao klabu ya Simba SC mchezo ambao utachezwa siku ya Jumamosi ya April 03 kuanzia majira ya saa 10:00 jioni kwenye dimba la Benjamini Mkapa.

Kwenye msafara huo beki wa kulia Djuma Shabani, hayupo kufuatia tarifa kutoka DR Congo kueleza kuwa anakabiliwa na majereha ya mguu,alioyapata akiwa kwenye majukumu ya timu ya taifa ya DR Congo.

Wachezaji 24 ambao wapo kwenye msafara utakaowasili Tanzania kwa ajili ya mchezo dhidi ya Simba SC Magolikipa wapo watatu Simon Omossola, Landu Mavamba na Nathan Mabruki.

Mabeki wanane: Vivien Assie, Ousmane Ouattara, Arnaud Akpako, Guy Mfingi, Patou Ebunga, Blessed Wahola, Jacques Mangoba na Michael Wango.

Viungo wanane: Papy Tshishimbi, Sidi Yacoub, Pascal Mbarga, Amédé Masi, Wonderful Kikasa, Never lie, Ricky Tuelenge na Jeremy Mumbere.

Washambuliaji  watano: Jeremy Mbuyi, Glody Lilepo, Ducapel Moloko, Filston Kalala na Eric Kabwe.

Simba SC inaongoza msimamo wa Kundi A kwa kufikisha alama 10, ikifuatiwa na Al Ahly yenye alama 7, AS Vita inashika nafasi ya tatu kwa kumiliki alama 4 na AlMerrikh wanaburuza mkia kwa kupata alama moja kwenye michezo minne waliocheza.

Mashabiki 10,000 kushuhudia Simba Vs AS Vita
Wateule wa Rais Samia kuapishwa leo