Mkazi wa kijiji cha Usagara, wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, Dementilia Saidia (22) amehukumiwa kifungo cha nje miezi mitatu kwa kujaribu kujiua kwa kujinyonga na kitenge kinyume cha sheria kifungu cha 217 baada ya kukataliwa na aliyempa ujauzito.

Akisomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Misungwi, Eric Marley na mwendesha mastaka wa Polisi Ramsoney Salehe amesema katika kijiji cha Usagara saa saba mchana Januari 28 mwaka huu mshtakiwa Dementilia Saidia akiwa ni mtumishi wa ndani kwa Melesiana Marco(35) alijaribu kujinyonga kwa kujifunga kitenge shingoni na kujining’iniza kwenye kenchi na kuokolewa.

Baada ya mtuhumiwa kusomewa shtaka Kaimu Marley alimuuliza kama kweli mtuhumiwa alitenda kosa hilo baada ya mwajiri wake kumfukuza alipobaini kuwa ana ujauzito wa miezi mitatu.

”Nilichanganyikiwa nikaona nijinyonge kwani mwajiri ananifukuza nyumbani na aliyenipa mimba ananikataa” amesema Dementilia

Mara baada ya Mahakama kumsikiliza mtuhumiwa kwa kuwa ana ujauzito wa miezi mitatu na ukubwa wa tatizo ilimfunga kifungo cha nje miezi mitatu na kipindi chote atakuwa chini ya Maofisa Ustawi wa jamii kwa uangalizi wa karibu.

Makala: Kinachompa Membe ujasiri, 'jeuri' mbele ya wembe unaokata, ‘siri ni silaha?’
Tanzania, Ethiopia wajadili kukomesha uhamiaji haramu