Mchuuzi wa mtaani mwenye ulemavu raia wa Nigeria, Alika Ogorchukwu amepigwa hadi kufa huku mashahidi wakirekodi shambulio hilo lililotokea kwenye barabara kuu ya maduka nchini Italia, bila kutoa msaada.
Mauaji ya Ogorchukwu, yamewashtua watu wengi wakiwemo raia wa nchi hiyo ya Italia, huku video za tukio hilo zikisambaa kwa kasi mitandaoni na kuchapishwa katika tahariri za magazeti, zilizozungumzia tukio hilo kwa kulihusisha na ubaguzi wa rangi.
Mbali na raia, pia Wanasiasa wengi wameoneshwa kuumuzwa na tukio hilo ingawa kumeibuka kwa wasiwasi uwa mauaji hayo yanaweza kutumika kama kichocheo cha ubaguzi kabla ya uchaguzi wa kitaifa nchini Italy mwezi Septemba, 2022.
Ogorchukwu, alikumbwa na mkasa huo baada ya kupeleka bidhaa zake kwa Muitaliano Filippo Ferlazzo na Kisha kuondoka na baadaye Ferlazzo alimfuata kisha kuchukua fimbo yake ya kutembelea na kisha kumpiga hadi kufa.
Shambulio hilo linadaiwa kutokea eneo la Civitanova Marche, mji wa pwani ya Adriatic, ambapo Februari 2018, mtetezi wa mrengo wa kulia aliwapiga risasi na kuwajeruhi wahamiaji sita wa Kiafrika katika eneo la karibu la Macerata.
Miaka miwili kabla ya hapo, mwanamume mmoja wa Nigeria pia aliuawa katika eneo la Fermo, ambalo liko upande wa kusini, baada ya kujaribu kumtetea mke wake dhidi ya matusi ya kibaguzi.
Aliyeteuliwa atenguliwa kabla ya kuapishwa