Waziri wa Usalama wa Ndani nchini Kenya, Prof Kithure Kindiki amefungua rasmi awamu ya pili ya shughuli ya upasuaji wa maiti zilizofukuliwa kutoka kwa msitu wa Shakahola huku idadi ya watu waliothibitishwa kufariki ikiwa ni 241.

Zoezi hilo la upasuaji, linafanyika katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali Kuu ya Malindi na itaongozwa na mwanapatholojia mkuu wa serikali Dkt Johansen Oduor ambaye atakuwa akitoa taarifa saa kumi na moja jioni.

Jumla ya miili 129 itafanyiwa upasuaji kubaini kilichosababisha vifo vya watu hao wanaoaminika walikuwa wafuasi wa mahubiri ya Pasta Paul Mackenzi wa kanisa la Good News International. Kwenye awamu ya kwanza ni miili 112 iliyofanyiwa upasuaji.

Waziri wa Usalama wa Ndani nchini Kenya, Prof Kithure Kindiki akiongea mbele ya vyombo vya Habari.

Hata hivyo, Waziri Kindiki amesema kikosi cha uokozi kilipata mifupa mikavu ya watu watano, iliyopatikana baada ya kusitishwa kwa ufukuaji zaidi wa makaburi ndani ya shamba hilo ambapo mtu mmoja aliyeokolewa alifariki akiwa hospitalini kutokana na kugoma kula.

Hadi sasa watu waliookolewa ni 91, huku Maafisa na wataalam wakikusanya sampuli za vinasaba vya DNA kutoka kwa familia 93 ambapo Familia 19 zimeunganishwa na wapendwa wao huku jumla ya watu 34 wakikamatwa kutokana na tukio hilo.

Mifumo utatuzi migogoro ya ardhi kuimarishwa - Dkt. Mabula
Wanne akiwemo Sangoma washikiliwa kwa mauaji, ubakaji