Malipo ya bima hayapo kwaajili ya kumnufaisha mtu zaidi ya hasara halisi aliyoipata. Malipo ya hasara hutegemea thamani ya kitu uliyotamka (declare) wakati wa kukata bima.

Thamani hii wakati wa malipo hupungua kutokana na kitu kinachoitwa ‘excess’ Yaani kama wakati wa kukata bima ulisema gari lako lina thamani ya TZS 8,000,000.

Basi gari ikipata ajali utalipwa 8,000,000- (kiwango kilichowekwa kama mchango wako mwenyewe kwenye kurekebisha hiyo hasara). Kiwango hiki huwekwa na kampuni ya bima kwa mfumo wa asilimia au tarakimu halisi.

Excess ni nini?

Excess ni kiwango kinachowekwa na kampuni ya bima ambacho kama chombo kilichokatiwa bima kitapata ajali basi Bima wataanza kulipa kiasi kilichozidi kiwango kilichowekwa. Ikimaanisha kama hasara ni chini ya kiwnago hicho bima hawatalipa. Unatakiwa hasara hiyo uibebe wewe mwenyewe.

Mfano: Mkataba wa bima unaweza kusema ndugu XYZ kwa kulipa premium(ile hela unayolipa kununua bima) ya TZS 300,000, Kampuni ya bima inaahidi kumlipa XYZ kiasi kilichokatiwa bima pungufu ya Asilimia 2 ya kiwango hicho.

Hii ina maana kwamba bima watakulipa 7,840,000 wakiwa wametoa shilingi 160,000 ambazo ni sawa na 2% ya thamani iliyokatiwa bima(insured sum) au kama katika hiyo bima excess iko katika tarakimu halisi, mfano 500,000. Ina maana watakulipa 7,500,000.

Hivyo ni vizuri unapotaka kukata bima ukaelewa “excess” itakuwa ni shilingi ngapi. Kwa kawaida jinsi unavyolipa premium ndogo ndivyo unavyokuwa na excess kubwa. Kumbe jinsi unavyolipa premium kubwa ndivyo unavyokuwa na excess ndogo.

“Sasa wee nenda kakate bima ya gari lenye thamani ya shilingi 15,000,000 halafu sema lina thamani ya shilingi 7,000,000 ili ulipe premium ndogo. Ikitokea ajali usitegemee kulipwa 15,000,000.”

Kwanza kampuni ya bima ikigundua uliwadanganya gari lilikuwa na thamani ya 15m wewe ukasema 7m, wanaweza wasikulipe kabisaa, maana utakuwa umekiuka wajibu wako mkuu wa kuwa muwazi na mkweli(duty of utmost good faith aka uberrimae fidei).

Japo hilo halitokei mara nyingi kwakuwa kama ulitaja thamani ndogo, kitu ambacho kitaalamu kinaitwa “under insurance”, watatumia principle ya average ili kupata watakachokulipa. Hizi ni baadhi tu ya sababu nyingi zinazoweza kumfanya mtu asilipwe bima yake au aone kama amepunjwa baada ya kupata hasara.

Naamini nimekuongezea maarifa – Usalama Barabarani ni Jukumu Letu Sote.

Kutoka katika ukurasa wa RSA Tanzania.

Youssouph Dabo aubana uongozi Azam FC
Azam FC: Dakika 180, alama 06