Kocha Mkuu mpya wa Azam FC, Youssouph Dabo amependekeza kupatiwa msaidizi wake ndani ya timu hiyo atakayeshirikiana naye wakati atakapoanza majukumu msimu ujao.

Dabo raia wa Senegal alitambulishwa rasmi kuifundisha timu hiyo Mei Mosi mwaka huu akichukua nafasi ya Kali Ongala ambaye anaendelea kusimamia hadi mwisho wa msimu huu.

Kwa upande wa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Abdulkarim Amin ‘Popat’ amesema kwa sasa wako kwenye maandalizi ya kumalizia msimu na baada ya hapo wataendelea na programu za msimu ujao hivyo mambo yote yanayohusu mabadiliko kwenye benchi la ufundi yatajadiliwa na kupatiwa ufumbuzi baadae.

Hata hivyo imefahamika kuwa endapo Dabo ataletewa msaidizi haitoweza kuathiri nafasi ya Kali Ongala kwani kocha huyo ataendelea na majukumu yake ya kocha wa washambuliaji.

Dabo ametua kwenye timu hiyo baada ya kuachana na ASC Jaraaf de Dakar huku akikumbukwa zaidi baada ya kuifundisha Teungueth iliyokuwa na staa wa Simba, Pape Sakho na Malickou Ndoye wa Azam.

Rais samia, Museveni watembelea mradi wa Umeme Mbarara
Usiyoyajua kuhusu malipo ya Bima ajali vyombo vya moto