Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, linawashikilia watu wanne akiwemo mganga wa kienyeji kwa tuhuma za ubakaji, mauaji na kukutwa na nyeti za mwanamke katika kijiji cha Bugumangala kilichopo Wilaya ya Magu.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Willbroad Mutafungwa
amesema jeshi la Polisi lilipokea taarifa za mauaji ya Ester Lukoni (51), mkazi wa kijiji cha Bugumangala Mei 10, 2023 ambaye aliuawa kisha kukatwa sehemu zake za siri na mwili wake kutelekezwa katika shamba la mihogo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Willbroad Mutafungwa.

Amesema, “Katika tukio hilo ilionekana kuwa marehemu aliingiliwa kimwili kabla ya mauaji hayo ya kikatili, kwani katika eneo la tukio ulipatikana mpira wa kiume (kondomu) ambao ulikuwa umetumika. Tukio hilo lilifanywa na watu ambao hawakuwa wamefahamika kwa wakati ule.”

Ameongeza kuwa, mmoja wa watuhumiwa hao ambaye ni mganga wa kienyeji alipokea sehemu za siri za marehemu na kuikausha kwa moto kisha akaisaga kwa ajili ya matumizi ya uganga ambayo yalihusisha imani za kishirikina na watuhumiwa wamekiri kuhusika na mauaji hayo.

Awamu ya pili upasuaji maiti zilizofukuliwa yaanza
Rais samia, Museveni watembelea mradi wa Umeme Mbarara