Uongozi wa mabingwa wa kombe la shirikisho Tanzania bara (ASFC) Azam FC umesema kwa sasa bado una mkataba na beki kutoka nchini Ghana Yakub Mohamed ambaye ameanza kuhusishwa na mipango ya kuhamia kwa mabingwa wan chi Simba SC.

Yakub amekua katika kiwango kizuru tangu alipotua Chamazi, na chini ya utawala wa makocha waliopita Azam FC amekua chaguo la kipekee kwenye kikosi cha kwanza cha mabingwa hao wa kombe la shirikisho kutokana na ubora wake.

Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin “POPAT” amesema kuwa bado Yakub ni mali ya Azam FC kwa sasa, hivyo ikiwa kuna timu ambazo zinaiwinda saini yake ni lazima zifuate utaratibu.

“Yakub ana mkataba mrefu ndani ya Azam FC kwa sasa, hivyo ikiwa kuna timu ambazo zinahitaji saini yake naimani kwamba zinatambua utaratibu ulivyo na namna ya kufanya ili kupata saini za wachezaji wetu.”

Mkataba wa Yakub ndani ya Azam FC ni wa muda wa miaka miwili ambapo aliongeza mkataba huo msimu uliopita akiwa na mkataba wa mwaka mmoja mkononi, ambao unameguka mwishoni mwa msimu huu hivyo ataanza kuishi ndani ya mkataba mpya alioongeza msimu uliopita.

Gharama za kutengeneza ‘dawa’ maabara zawekwa wazi
Kilomoni aibuka, ahoji nguvu ya wanachama Simba SC