Timu  ya Azam iliyoenda Zambia kushiriki michuano maalum ya maandalizi imeanza mashindano hayo kwa kutoka sare ya mabao 1-1 na timu ya Zesco United.

Mabingwa wa Zambia, Zesco United walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa mshambuliaji wa kimataifa wa Kenya, Jesse Were.

Bao hilo lilidumu hadi kipindi cha mwili mwishoni wakati mshambuliaji  Kipre Tchetche alipoisawazishia Azam kwa kuunganisha mpira wa kona iliyochongwa na Ramadhani Singano katika dakika ya 90 ya mchezo.

Pambano la pili la michuano hio linawakutanisha wenyeji Zanaco na mabingwa wa Zimbabwe, Chicken Inn.

Enyimba FC Wagoma Kuja Tanzania
Luis Suarez Bado Ana Ndoto Za Kurejea Anfield

Comments

comments