Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya kombe la shirikisho Azam FC, wamethibitisha hadharani wapo kimataifa zaidi baada ya kuvaa mavazi maalum ya safari kama inavyokua kwa timu nyingine za barani Ulaya.

Azam FC wamesafiri muda mchache uliopita kuelekea Afrika Kusini, kwa ajili ya mchezo wa mzunguuko wa pili wa hatua ya mtoano wa michuano ya kombe la shirikisho la soka barani Afrika dhidi ya Bidvest utakaochezwa mwishoni mwa juma hili.

Wachezaji pamoja na viongozi wa Azam FC, wameonekana wakiwa wametinga vazi la suti ambalo ni maalum kwa safari yao ya hii leo, kuelekea Johannesburg.

azam 02 azam 03 azam 04

Mbali na kutinga vazi hilo, wachezaji pamoja na viongozi wa klabu hiyo iliyomaliza katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara msimu uliopita, walionekana kuwa na furaha.

Azam FC, wamesafiri wakiwa na kikosi cha wachezaji 24, sambamba na viongozi wa benchi la ufundi pamoja na viongozi wa utawala.

Picha: Rais Magufuli amtembelea Maalim Seif
Mwamuzi Wa Kike wa 'Simba Na Yanga' Kuchezesha Kombe La Dunia