Azam FC asubuhi ya leo imetua kwenye uwanja wa ndege wa Songwe jijini Mbeya na kupanda basi kwenda Songea kuwavaa wenyeji Majimaji katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mchezo huo utachezwa Jumapili ya keshokutwa kwenye dimba la Majimaji Songea.

Azam ilitua Mbeya saa 3 asubuhi na kufuatwa na basi lao kwa ajili ya safari ya kwenda huko Songea.

Kwa kawaida basi la Azam hutangulia mapema sehemu husika na kisha hutumika kuwapokea wachezaji pindi watumiapo usafiri wa ndege hasa ikitokea kwamba mechi inachezwa mikoa ya mbali na Dar es salaam.

Zifuatazo ni picha mbalimbali zikionyesha jinsi Azam ilivyopokewa na basi lao jijini Mbeya asubuhi ya leo.

Game Ya Kihistoria Imechezwa Salama Wa Salmini Nchini Somalia
Guus Hiddink Awashiwa Taa Ya Kijani Stamford Bridge