Historia imeandikwa katika ulimwengu wa soka Somalia baada ya mechi ya nyumbani kuonyeshwa moja kwa moja kwenye runinga.

Klabu ya wanajeshi ya Horseed ililaza klabu ya polisi ya Heegan FC 2-1 katika mechi hiyo, iliyokuwa ya fainali ya Kombe la Jenerali Da’ud.

Rais wa shirikisho la soka la Somalia Abdiqani Said Arab alisema kupeperushwa kwa matangazo ya mechi hiyo ni ufanisi mkubwa.

Taifa hilo bado linajikwamua kutoka kwa mapigano ya takriban ya miongo miwili.

Wapiganaji wa Kiislamu wa al-Shabab, ambao wameamuru wachezaji wa soka wawe wakivalia suruali ndefu bado wanadhibiti maeneo mengi.

Said Arab aliongeza: “Tumekuwa na ndoto ya kuona mechi zetu zikionyeshwa moja kwa moja kwa muda mrefu. Huku ni kutimia kwa ndoto.”

Amesema sasa watajaribu kuwa wakionyesha mechi moja kwa moja.

Michuano ya kuwania kombe la Jenerali Da’ud ndiyo ya pili katika michezo kwa kuvutia mashabiki wengi nchini humo.

Shindano hilo hufanyika kila mwaka na limepewa jina hilo kutokana na mwanzilishi wa Jeshi la Somalia, Jenerali Da’ud Abdulle Hersi.

Jenerali Da’ud, aliyezaliwa 1924 katika kijiji cha Mareeg kusini mashariki mwa Somalia, alifariki mwaka wa 1965 na serikali ya Somalia imekuwa ikiandaa na kufadhili kombe hilo la soka tangu mwaka wa 1972.

Stand Utd Waapa Kuisimamisha Dar e salaam Young Africans
Azam FC Wawafuata Majimaji Mkoani Ruvuma