Uongozi wa Azam FC umeweka wazi kuwa kwenye michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara wanayocheza kwa sasa, wanahitaji alama tatu tu na mabao, kutoka kwa wachezaji wao.

Azam FC imetoka kumpa maumivu Simba SC kisha ikayahamishia kwa Ihefu FC kwa dozi ya mwendo wa mojamoja kwa timu hizo huku mfungaji wao akiwa Mshambuliaji kutoka Zimbabwe Prince Mpumelelo Dube.

Afisa Habari wa Azam FC Hasheem Ibwe amesema kuwa wanatambua uliopo kwenye kusaka matokeo lakini hilo haliwapi shida, kikubwa wanachohitaji ni alama tatu tu.

“Sisi ambacho tunakitaka kwenye michezo yetu ambayo tunacheza ni alama tatu tu, haijalishi tunacheza na mpinzani wa aina gani, jambo la muhimu ni ushindi na mabao.”

“Huwezi kupata alama bila kufunga, wapinzani wetu tunawaheshimu na tunawafuata kwa tahadhari kubwa lakini ambacho tunahitaji ni alama tatu.” amesema Ibwe

Azam FC itaendelea kuwa mwenyeji katika Uwanja wake wa Azam Complex-Chamazi jijini Dar es salaam kwa kuikaribisha Dodoma Jiji FC keshokutwa Jumatano (Novemba 09).

Azam FC ilikua mwenyeji katika michezo yake miwili iliyopita ikicheza dhidi ya Simba SC katika Uwanja wa Benjamin Mkapa na baadae ikaikaribisha Ihefu FC kwenye Uwanja wa Azam Complex-Chamazi.

Simba Queens yalamba milioni 565.4
AU yapendekeza msaada wa kifedha kwa Ukraine