Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya AU, Ursula von der Leyen anatarajia kupendekeza usaidizi kwa nchi ya Ukraine katika mwaka wa 2023 wa kuipatia hadi dola bilioni 18.

Von der Leyen, amemfahamisha rais wa Ukraine, Volodymyrr Zelenskiy kuhusu mipango yake katika mazungumzo ya simu jana Jumapili (Novemba 6, 2022), juu ya hatua hizo.

Fedha ya Ukraine. Picha ya Frank Hammerschmidt.

Kiasi jumla kitakachopelekwa Ukraine, kinaratajia kuwa sawa na hadi dola bilioni 1.5 kila mwezi, katika mwaka ujao wa fedha ili kiweze kuisaidia nchi hiyo iliyoharibiwa na vita.

June 2022, Viongozi wa Umoja wa Ulaya, waliamua kuipatia Ukraine msaada wa dola bilioni 9 ili kushughulikia mahitaji yake ya haraka ya kifedha, kufuatia uvamizi wa Urusi nchini humo.

Azam FC yaichimba mkwara Dodoma Jiji FC
Bodi ya ushauri kuipeleka Tanzania AFCON 2027, Kombe la Dunia 2030