Siku moja baada ya kutoka sare ya 2-2 na JKT Ruvu, Azam FC imekumbana na balaa lingine la kupokwa pointi tatu na mabao matatu kwa kosa la kumtumia beki wao, Erasto Nyoni aliyekuwa na kadi tatu za njano.

Taarifa za uhakika zinasema katika mchezo namba 156 iliyozikutanisha Mbeya City dhidi ya Azam kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, Azam FC ilimchezesha Nyoni kinyume na sheria huku wakitambua kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Adhabu hiyo inafuatia ushindi wa Azam wa mabao 3-0 iliyoupata Februari 20 mwaka huu kwenye dimba la Sokoine Mbeya huku ndani yake akichezeshwa Erasto Nyoni aliyekuwa na kadi tatu za njano.

Licha ya kushinda Azam FC wamepoteza mchezo huo na sasa Mbeya City imepewa pointi tatu na mabao matatu huku benchi la ufundi la Azam FC likionywa kuwa makini ili jambo hilo lisiwatokee tena.

Maamuzi hayo yanaendelea kuwapa nafasi Young Africans kuusogelea ubingwa wa ligi kuu ya soka Tanzania bara msimu wa 2015-16.

CCM: TAARIFA YA KUKANUSHA UZUSHI WA VYOMBO VYA HABARI
Mahakama Kuu yamalizana na Kafulila