Mahakama Kuu Kanda ya Tabora imesema kuwa imekamilisha hatua zote za kusikiliza kesi ya uchaguzi iliyofunguliwa na aliyekuwa mbunge wa jimbo la Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi) dhidi ya aliyetangazwa kuwa mshindi katika uchaguzi wa mwaka jana, Hasna Mwilima (CCM).

Jaji Ferdinand Wambali, aliyesikiliza kesi hiyo amesema kuwa Mahakama hiyo imefunga ushahidi wote baada ya kusikiliza pande zote mbili na inatarajia kutoa hukumu rasmi Mei 17 mwaka huu.

Alisema kuwa hivi sasa Mahakama hiyo inahitaji muda wa kupitia kwa makini ushahidi wote na vielelezo vilivyowasilishwa Mahakamani hapo ili kuhakikisha inatoa hukumu ya haki.

Katika kesi ya msingi, Kafulila anapinga ushindi wa Mwilima akidai kuwa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo alimpokonya ushindi wake.

Walalamikiwa katika kesi hiyo ni Mbunge wa jimbo hilo, Hasna Mwilima, Msimamizi wa Uchaguzi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliyeiwakilisha Tume ya Taifa ya uchaguzi.

Azam FC Yapunguziwa Point Tatu Na Kuiacha Young Africans Ikichekelea
Zimbabwe kutoa Dola yake yenye thamani sawa na Dola ya Marekani