Kocha wa Mbeya City mmalawi Kinnah Phiri ametaja kasoro kadhaa zilizosababisha timu hyake ipoteze mchezo wa ugenini dhidi ya Simba kwa kukubali kufungwa mabao 2-0 kwa mara ya kwanza kwenye uwanja wa taifa.

Phiri ambaye ni mgeni katika timu ya Mbeya City amesema wachezaji wake kushindwa kutumia vyema nafasi zilizopatikana kulifanya washindwe kupata bao huku akisema uzoefu wa wachezaji wa Simba ndiyo ulioamua game hiyo.

“Tulitakiwa kufanya vizuri zaidi tulipata nafuasi za kufunga lakini wachezaji hawakutimiza majukumu yao lakini hivyo ni vitu ambavyo nitavishughulikia kama kocha”, anasema kocha huyo raia wa Malawi ambaye alikuwa akifundisha soka nchini Afrika Kusini kabla yakutimuliwa na kuhamia Bongo.

“Mashuti mawili langoni siyo kitu kizuri kwa timu, tulitarajia kupiga mashuti mengi zaidi lakini ukiangalia mchezo mzima hata kwa upande wa Simba hawakupata nafasi ya kupiga mashuti mengi kwetu lakini walitufunga kwasababu ya uzoefu wao”.

“Kwa ujumla mchezo ulikuwa mzuri Simba walicheza vizuri na sisi tuliheza vizuri na sifikirii kama Simba watasema wamepata ushindi kirahisi ulikuwa ni mchezo mgumu kwa upande wao pia lakini walitumia vizuri nafasi walizopata huku sisi tukishindwa kutumia nafasi”.

Licha ya kupoteza mchezo huo, Mbeya City ilionesha kiwango bora kwenye mchezo dhidi ya Simba huku wachezaji Kenny Ally pamoja na Joseph Mahundi wakionesha viwango vya hali ya juu.

Ligi Kuu Kuendelea Katikati Ya Juma
Ofisi za CUF zachomwa moto Zanzibar