Watu ambao hadi sasa hawajajulikana wamechoma moto Ofisi za matawi matano ya Chama Cha Wananchi (CUF) zilizopo Pemba na Unguja usiku wa wa kuamkia jana.

Tukio hilo limetokea ikiwa ni siku chache baada ya kuripotiwa mlipuko wa kitu kinachosadikika kuwa ni Bomu, katika maskani maarufu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) yaliyoko Unguja.

Jeshi la polisi limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa tayari limeanzisha uchunguzi kubaini waliohusika ili wachukuliwe hatua za kisheria.

“Ni kweli kuna hilo tukio ingawa kwa sasa nipo safari kuelekea Unguja na tayari nimeagiza kuanza kwa uchunguzi wa matukio haya ili wahusika waweze kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria,” Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, Hassan Nassir alisema.

Kamanda Nassir alieleza kuwa hawezi kulihusanisha moja kwa moja tukio hilo na masuala ya kisiasa lakini huo ni uhalifu kama ulivyo uhalifu mwingine.

Baada Ya Kibano Cha Simba, Kinnah Phiri Ajivunia Kikosi Chake
Lulu, Richie waibeba Bongo Movies Kimataifa, Wanyanyua Tuzo AMVCA