Mtoto bahati juma mwenye umri wa miaka miwili ameuawa na baba yake mzazi  mkoani Kagera kwa kumchoma moto usoni na makalioni baada ya mtoto huyo kujisaidia haja kubwa kitandani.

Jeshi la Polisi mkoni Kagera linamshikilia Baba mzazi wa mtoto huyo Juma Daniel mkazi wa kijiji cha kazingati kata ya Keza wilayani Ngara.

Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Revocatus Malimi, amesema kuwa Baba huyo alikwishatengana na mama mzazi wa mtoto huyo na kuoa mke mwingine.

Daniel anadaiwa kumuuwa mwanaye huyo kwa kumchoma moto usoni na makalioni na kumjeruhi kwa kitu chenye ncha kali sehemu za haja kubwa, baada ya mtoto huyo kujisaidia haja kubwa kitandani wakati wamelala.

Aidha Kamanda Malimi amesema kwamba alifanyiwa kitendo hicho cha kikatili Disemba 27, 2019 na hakumpelekwa hospitali badala yake alianza kumtibu kienyeji nyumbani, na baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya baba huyo alitoroka.

Video: Waziri akuta kondomu zikiwa zimeanikwa juani hospitalini
Video: Vyombo, nguo, magodoro vyasombwa, wananchi walia umaskini

Comments

comments