Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki – Moon, amempongeza Rais John Magufuli kwa kuchaguliwa kuiongoza serikali ya awamu ya tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kupitia pongezi zake zilizotolewa jana na Ikulu kupitia yombo vya habari, Ban Ki-Moon amepongeza mchakato wa kidemokrasia uliotumika kumpata Rais Magufuli kwa amani na utulivu.

“Uchaguzi wa mwaka 2015 ni uthibitisho wa wazi na dhamira ya muda mrefu ya watanzania kwa demokrasia, amani na utulivu. Nina imani kuwa masuala ya uchaguzi yaliyobakia yatashughulikiwa kupitia utaratibu wa sheria uliopo kwa njia ya amanina uwazi,” alinukuliwa.

Alieleza kuwa anatambua kuwa serikali ya Rais Magufuli itaendeleza juhudi za kupambana na umasikini  na kuhakikisha uwepo wa amani na utulilivu katika ukanda wa Afrika Mashariki, na kueleza kuwa Umoja wa Mataifa utaendelea kuunga mkono juhudi hizo.

“Nathamini ushirikiano uliopo kati ya Umoja wa Mataifa na nchi yako katika kuendeleza malengo ya UN, nakutakia mafanikio katika kutekeleza shughuli zako,” taarifa hiyo ilimkariri.

 

Mbinu za Ukawa Kumtumia Lowassa Uspika Zanaswa
DJ Mwenye Umri Wa Miaka Mitatu Ashinda Shindano La ‘SA Got Talent’