Serikali imeanza mazungumzo na wawekezaji kufufua mradi wa Bandari ya Bagamoyo pamoja na ule wa Mchichuma na Liganga

Hayo yamesemwa na Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassani leo Juni 26, 2021 wakati akifungua mkutano wa 12 wa Baraza la Taifa la Biashara(TBNC) Ikulu Jijini Dar Es Salaam.

“Bagamoyo tunakwenda kuanza mazungumzo na taasisi iliyokuja kwa ajili ya mradi huu ili tuifungue na tuende nao kwa faida yetu. Taarifa zilizopo duniani chuma imepanda bei ni wakati mzuri wa kuharakisha kuufanya mradi huu” amesema Rais Samia.

“Nilishatoa maelekezo nadhani sekta husika wanaendelea na mazungumzo na wawekezaji wa Mchuchuma na Liganga kuona tatizo ni nini hasa. Serikali inaweza kujitoa hadi wapi na mwekezaji anaweza kujitoa hadi wapi ili mradi ufanye kazi.”

Itakumbukwa kuwa Rais wa awamu ya tano, Hayati John Magufuli aliwahi kukaririwa akisema ujenzi wa bandari hiyo una masharti magumu ya mwekezaji ndio sababu ya kusuasua kutekelezwa.

Rais Samia atoa agizo kwa Wakuu wa Mikoa, Wilaya
Waziri amtimua kazi meneja