Kanuni ya bao la ugenini imeibeba AS Monaco ya nchini Ufaransa na kuipeleka kwenye hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.

AS Monaco wamefanikiwa kusonga mbele katika michuano hiyo kufuatia ushindi wa mabao matatu kwa moja waliouvuna usiku wa kuamkia leo dhidi ya matajiri wa jijini Manchester (Man City).

AS Monaco walipambana katika mchezo huo uliofanyika Stade Louis II, na kupata ushindi huo kupitia kwa Kylian Mbappe Lottin, Fábio Henrique Tavares na Tiemoue Bakayoko huku bao la kufutia machozi la Man City likifungwa na Leroy Sane.

Kabla ya mchezo huo Man City walikua wakiongoza kwa mabao matano kwa matatu, hali ambayo iliwalazimu AS Monaco kutafuta ushindi wa mabao mawili kwa sifuri ama zaidi.

Kufutia matokeo yaliyopatikana kwenye mchezo wa mkondo wa pili, timu hizo zimetoshana nguvu kwa sare ya mabao sita kwa sita, lakini kanuni ya bao la ugenini inawabeba AS Monaco ambao wanasonga mbele.

Mabao matatu yaliyopatikana katika mchezo wa mkondo wa kwanza yanakua mtaji mzuri kwa AS Monaco kutimiza lengo la kuwa sehemu ya timu nane zilizotinga kwenye hatua ya robo fainali.

Bayer Leverkusen Yashindwa Kutimiza Lengo
Video: Diamond amshauri Makonda kuhusu ‘wanaomsema’, vita ya dawa za kulevya