Rais wa FC Barcelona, Josep Maria Bartomeu amesisitiza kuwa na imani na mshambuliaji mahiri wa klabu hiyo Lionel Messi, kuuwahi mchezo wa novemba 21, ambapo watapambana na Real Madrid.

Bartomeu, amesisitiza jambo hilo, kutokana na hali tete iliyotanda FC Barcelona, ambapo inaaminiwa huenda Lionel Messi akawa nje ya kikosi kitakachosafiri kuelekea mjini Madrid, mwishoni mwa juma lijalo kutokana na majeraha goti yanayomkabili.

Amesema mshambuliaji huyo anaendelea kupatiwa matibabu na jopo la madaktari klabuni hapo, na taarifa anazoendelea kuzipokea kila siku, zinampa matumaini ya kumuona Messi mjini Madrid.

Katika hatua nyingine, Bartomeu, amewataka mashabiki wa FC Barcelona kuwa na ustahamilivu katika kipindi hiki cha kusubiri hali ya mshambuliaji huyo ambaye alipatwa na maumivu ya goti, wakati wa mchezo wa ligi dhidi ya Las Palmas, uliochezwa mwezi septemba.

Hata hivyo, makadirio yaliyotangazwa na wahusika wa utabibu huko Camp Nou, yalionyesha Lionel Messi huenda akawa fit wakati wa mchezo wa El Classico, hivyo ni jambo la kusubiri na kuona kama atakuwa sehemu ya kikosi cha FC Barcelona siku hiyo.

FC Barcelona, wataelekea katika mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu kubwa karibu na mashabiki wa soka duniani kote, huku wakiwa na ujasiri mkubwa, kutokana na kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi ya nchini Hispania kwa tofauti ya point tatu dhidi ya mahasimu wao Real Madrid.

Kikwete: Taifa Stars Mpeni Heshima John Magufuli
Masanja Mkandamizaji Ashindwa Kura Za Maoni Ludewa